WiFi Billing System

Kuhusu Mfumo wa WiFi Billing

Mfumo wetu wa WiFi Billing unakuwezesha kubadilisha mtandao wako wa internet kuwa chanzo cha mapato. Ni mfumo unaofaa sana kwa wenye frame, migahawa, hoteli, nyumba za kulaza wageni (lodges), au maeneo ya mitaani yenye mzunguko mkubwa wa watu.

Faida na Sifa Kuu za Mfumo:

  • Uuzaji wa Vocha: Kutengeneza na kuchapa vocha za muda (mfano: Saa 1, Masaa 12, Siku 1, au Mwezi 1).
  • Malipo ya Mtandaoni: Wateja wanaweza kulipia bando moja kwa moja kupitia M-Pesa au Namba ya Malipo na kuunganishwa hapo hapo.
  • Udhibiti wa Kasi (Bandwidth Control): Mfumo unagawanya spidi vizuri ili kila mtumiaji apate mtandao wa kasi sawa.
  • Ripoti za Mapato: Utakuwa na uwezo wa kuona takwimu za mauzo na idadi ya wateja waliounganishwa kila siku.

Jinsi Inavyofanya Kazi:

  1. Mteja akiwasha WiFi ya simu yake, ataona jina la WiFi yako na kuunganisha.
  2. Ukurasa wa kuingiza Vocha au Kulipia utafunguka mara moja kwenye simu yake (Captive Portal).
  3. Akishaingiza vocha au kulipia, mfumo unamruhusu kutumia mtandao kulingana na muda au MB alizonunua.

Je, unahitaji mfumo huu kwa ajili ya biashara yako?

Wasiliana nasi leo upate ushauri wa bure na kuwekewa mfumo huu kwa haraka.

Agiza Mfumo Hivi Sasa

Huduma Zingine